The House of Favourite Newspapers

Tambwe amvaa Kiiza, ampiga mikwara

0

download

Mshambuliaji wa Yanga Mrundi, Amissi Tambwe.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
LICHA ya ‘hat trick’ aliyoipiga mshambuliaji mpya wa Simba Mganda, Hamis Kiiza, lakini mshambuliaji wa Yanga Mrundi, Amissi Tambwe, amemwambia kuwa hawezi kutwaa tuzo ya mfungaji bora msimu huu.

Mganda huyo, wikiendi iliyopita aliandika rekodi ya kwanza kwenye msimu huu wa ligi kuu ya kupiga ‘hat trick’ kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1.

‘Hat trick’ hiyo aliyoipiga Kiiza imesababisha imuondoe Tambwe kileleni mwa chati ya wafungaji bora wa ligi hiyo ambapo walikuwa wanalingana na Mzimbabwe, Donald Ngoma kwa mabao matatu matatu.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa ‘hat trick’ hiyo aliyoipiga Kiiza haimfanyi yeye akatishe ndoto alizojiwekea za kutwaa ufungaji bora kwenye msimu huu.

Tambwe alisema, anapata matumaini zaidi ya kumzuia Kiiza kutwaa ufungaji bora.
Aliongeza kuwa, kikubwa alichokipanga yeye ni kuhakikisha anatumia kila nafasi anayoipata ndani ya uwanja kwa kufunga mabao ikiwemo mechi dhidi ya Simba watakayoicheza Jumamosi hii.

“Nimepata taarifa za Kiiza kufunga mabao matatu na kunitoa kwenye nafasi ya kwanza ya chati ya ufungaji msimu huu, nampongeza lakini kikubwa asijipe matumaini ya ufungaji bora.

“Kikubwa nilichokipanga mimi ni kuhakikisha ninamaliza ligi kuu nikiwa mfungaji bora, ninaamini hayo malengo pia anayo Kiiza.

“Lakini nikuhakikishie kuwa sitakubali kuacha ufungaji bora kwenye msimu huu baada ya kuukosa kwenye msimu uliopita ambao ulichukuliwa na Msuva (Simon),” alisema Tambwe.

Tambwe kwenye msimu wa 2013/14, alifanikiwa kutwaa ufungaji bora akipachika mabao 19 kabla ya msimu uliopita kuchukuliwa na Msuva.

Leave A Reply