The House of Favourite Newspapers

Tambwe Ana Hela Acheni, Anamiliki Toyota Land Cruiser V8 TD

Mshambuliaji wa Yanga Mrundi, Tambwe (wa tatu kutoka kulia)

HAKUNA ubishi mshambuliaji wa Yanga Mrundi, Tambwe ndiye mchezaji anayeongoza kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara wanaosukuma mkoko wa kifahari. Mrundi huyo aliyewahi kuichezea Simba na kutwaa ufungaji bora mara mbili akiwa wa timu hiyo na Yanga anamiliki gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 TD toleo la 2008.

Toyota Land Cruiser V8 TD.

Tofauti na mkoko huo, pia anamiliki gari lingine aina ya Toyota Mark X ambalo hilo wapo baadhi ya wachezaji wanaolisukuma kwenye Ligi Kuu Bara kama vile Erasto Nyoni na Shomari Kapombe wote wanaoichezea Simba. Spoti Xtra lilifanya mahojiano maalum na Tambwe kuzungumzia thamani ya gari hilo na kiasi cha fedha anachokitumia kuweka mafuta katika mizunguko yake.

 

Spoti Xtra ambalo linaongoza kwa mauzo kila Jumapili na Alhamisi, limegundua mengi ikiwemo kufuru anayoitumia katika fedha kupitia gari hilo ambayo yalikuwa hivi.

 

ALINUNUA WAPI?

“Baadhi ya watu wanajua kuwa hili gari langu nimenunua hapa wengine wanajua nyumbani Burundi, lakini ukweli ni kwamba niliagizia kutoka nchini Japani. “Baada ya kuliagizia lilifika Bandari ya Tanzania na kulitoa hapo nikalipeleka kwetu kulisajili na kukamilisha taratibu zingine ndio maana unaona lina namba za Burundi.

 

“Nikienda kwetu na kurudi huwa nalitumia,”anasema Tambwe.

 

ALILIKOMBOA KWA SH MIL. 3.5

“Baada ya kufika bandarini niliambiwa nilipie dola 1500 (zaidi ya Shilingi Milioni 3.5) kwa ajili ya kulipia kodi na malipo mengine,halikukaa sana. “Baada ya kulipa gharama hizo, nililisafirisha kutoka hapa jijini Dar es Salaam na kwenda Burundi kwa ajili ya kusajili namba ya nyumbani,”anasema Tambwe. Kiuhalisia gharama hizo zilizotumika kwa ajili ya kulitoa bandarini zinaweza kufanikisha usajili wamchezaji mmoja anayecheza pale Biashara FC, Alliance United, Lipuli au Coastal Union.

 

KANUNUA SH MIL.35.2 “Bei ni ya kawaida wala isiwaogopeshe ni dola 15, 000 (zaidi ya Shilingi Milioni 35.2) ndiyo nilizozitumia kununua gari hili
mnaloliona kutoka Japani. “Nasema ni bei ya kawaida kutokana na ndoto zangu nilizoweka za kumiliki la aina hiyo kwa gharama yoyote ile katika kufuraisha nafsi yangu ya moyo.

 

“Siku zote ninafanya kile kitu kinachohitaji moyoni mwangu, kama ilivyokuwa kwa kumiliki gari hilo ambalo ninaamini mimi pekee ninayelitumia.” Lakini kiasi hicho alichotumia Tambwe kinaweza kumsajili mchezaji wa Simba, Yanga na Azam. Mastaa wengi wa timu hizo wamesajiliwa kwa Shilingi Milioni 30 katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

 

MATENGENEZO ‘SEVISI’ 200, 000 “Hiyo ndiyo gharama ninayoitumia kwa ajili ya ‘sevisi’ na nimekuwa nikiifanya kutokana na kilomita ambazo nimekuwa nikitembea kuanzia 500. “Ukiangalia ni gharama kubwa kiukweli, lakini kutokana na thamani, hadhi ya hili gari ninalazimika kutumia kiasi hicho cha fedha kufanyia service kwa hofu ya kuingia gharama nyingine zitakazotokana na kuharibika.

 

TAIRI SH. 400, 000 “Hiyo ndiyo gharama niliyoitumia kununua tairi katika gari yangu, kama nilivyosema awali gari hili la gharama hivyo vyote unavyoviona katika hili gari ni gharama zikiwemo spea zake. “Hiyo ni tairi pekee, lakini bado rimu ambazo zenyewe ni bei tofauti na tairi ambayo nimesahau bei yake. Taa moja ya nyuma ya gari hilo ina thamani ya Sh.200,000.

 

MAFUTA NI SH. 50, 000 “Mafuta hayo nayatumia kwa siku moja pekee kwa maana nikitoka mazoezini kuanzia hapa nyumbani kwangu Sinza, Madukani kwenda Kurasini na kurudi, nikipiga misele yangu miwili kitaani mafuta yanakuwa yamemamalizika. “Hivyo, ninatakiwa niongeze mafuta mengine siku nyingine inayofuata kwa kuanzia kituo cha mafuta kabla ya kuanza safari nyingine ya kwenda mazoezini asubuhi.

 

“Kama nisipoongeza mafuta, basi gari lazima nilizimikie kutokana na gari hili kula mafuta mengi tofauti na gari langu la Mark X. Shilingi 50, 000 hiyo inaweza kutumika kama posho ya mchezaji anaekaa jukwaani wa Simba tofauti na wale wanaocheza ambao wenyewe wanavuta Shilingi 400, 000 kwa mechi wanayoshinda.

 

MUZIKI 200, 000 “Nimefunga muziki wa saizi ya katikati siyo mkubwa sana, na gharama nilizozitumia ndiyo hizo ambao utumia flashi na cd katika kusikiliza muziki nikiwa ninaendelesha,” anasema Tambwe

Comments are closed.