The House of Favourite Newspapers

Tambwe apata gonjwa la ajabu

AmissTambwe2Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

SIKU moja baada mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe kujiunga na kikosi cha timu hiyo akitokea kwao alikokuwa ameenda kwa ajili ya kuitumikia nchi yake hiyo katika michuano ya kimataifa, amekumbwa na balaa la aina yake.

Tambwe ambaye msimu uliopita aliifungia Yanga mabao 14 katika Ligi Kuu Bara, jana asubuhi aliamka akiwa na maumivu ya makali ya shingo wakati jana yake alikuwa fiti kabisa.

Hali hiyo ilimfanya ashindwe kuungana na wenzake katika mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, licha ya kuwemo eneo la tukio. Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe alisema hajui hali hiyo imesababishwa na nini kwa sababu alikuwa mzima kabisa tangu alipotua nchini Jumanne iliyopita ila jambo la kushangaza jana kaamka akiwa na maumivu makali ya shingo.

“Hata sijui maumivu haya yametokana na nini kwani shingo inauma sana hali inayonifanya nishindwe hata kumeza mate, nikifanya hivyo nahisi maumivu makali nyuma ya shingo.

“Kuhusu matibabu, tayari nimeshaanza lakini pia daktari wetu wa timu ameniandikIa dawa za kwenda kununua ili nimeze na kama kesho (leo) nitaamka vizuri, nitaungana na wenzangu kwa ajili ya mazoezi,” alisema Tambwe.

Alipoulizwa Daktari wa Yanga, Haruni Ally kuhusiana na tatizo hilo la Tambwe, alisema: “Inawezekana akawa amelala vibaya au hali ya hewa kwani alikokuwa, hali yake ya hewa ni tofauti na hii ya hapa Dar es Salaam.

“Hiyo pia inaweza kuwa sababu ya tatizo hilo, lakini kuna dawa ambazo nimempatia akatumi,e kama hali itazidi kuwa mbaya basi itabadi tukamfanyie uchunguzi zaidi,” alisema Ally.

Comments are closed.