The House of Favourite Newspapers

Tambwe arejea, Tshishimbi atoweka

Amisi Tambwe mwenye jezi namba 17 akiwa pamoja na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru
Wachezaji wa Yanga wakinyoosha misuli .

 

Wachezaji wa Yanga pamoja na makocha wakifanya maombi baada ya kumalizika kwa mazoezi kwenye Uwanja wa uhuru.

 

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amerejea rasmi ndani ya kikosi hicho na kuanza mazoezi huku straika mwenzake Mzambia Obrey Chirwa akikosekana mazoezini hapo pamoja na Kiungo Papy Tshishimbi akishindwa kuungana na wenzake baada ya kuchelewa kufika kutokana na gari lake kuharibika.

Yanga imeendelea na mazoezi yake uwanjani hapo baada ya hivi karibuni kufanya mazoezi ya Gym, Yanga wanajiandaa na michuano ya FA pamoja na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea hivi karibuni.

Comments are closed.