TAMBWE ATAJA SIRI YA MABAO YAKE YANGA

Mshambuliaji nyota wa Yanga Hamis Tambwe

AMISSI Tambwe amesema aliifunga Prisons kwa hasira sababu ya Simba. Mrundi huyo, alifikisha mabao manne aliyoyafunga tangu kuanza kwa msimu huu wakati walipoipiga Prisons mabao 3-1 huku akitupia mabao mawili.

 

Tambwe aliyewahi kuwa mfungaji bora kwenye misimu miwili ya ligi mabao yake mengine aliyafunga katika mchezo wa ligi na Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Tambwe alisema; “Tunajua tunapitia kipindi kigumu hivi sasa wachezaji wa Yanga kwa maana ya hali ya kiuchumi tuliyokuwa nayo, lakini hali hiyo haitufanyi kukata tamaa na badala yake kuendelea kuipambania timu kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu.”

 

“Na malengo yetu ni kuwanyang’anya ubingwa Simba waliouchukua katika msimu uliopita, hivyo basi nilichopanga ni kuendelea kuitumia kila nafasi nitakayoipata kufunga mabao.

 

“Mabao niliyoyafunga mechi na Prisons yametokana na kujituma kwangu na kutambua umuhimu wa ushindi huo ambao utawaacha mbali wapinzani wetu katika malengo yetu tuliyojiwekea ya ubingwa msimu huu,” alisema Tambwe ambaye hivi karibuni alifunga ndoa hapa nchini.

STORI NA WILBERT MOLANDI | SPOTI XTRA

Toa comment