Tambwe: Fei Toto ni Mchezaji Hatari Yanga

ALIYEKUWA Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amefunguka kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri na hatari zaidi kwenye kikosi cha Yanga.

Tambwe ambaye aliwahi kuitumikia Yanga kwa msimu huu wa 2021/22 anakipiga ndani ya Klabu ya DTB ambayo inashiriki michuano ya Championship ikiwa inatafuta nafasi ya kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Nyota huyo wikiendi iliyopita aliifungia DTB mabao manne dhidi ya Lyon ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Championship.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa: “Kwa kikosi cha Yanga Fei Toto ni mchezaji hatari, niliwahi kucheza nae ila mwanzo alikuwa anacheza namba sita nafasi ambayo ilikuwa inamfanya acheze faulo nyingi ila kwa sasa anacheza namba kumi wamempatia sana kwani ni mchezaji ambaye anapenda kuuchezea mpira.”

LEEN ESSAU, Dar es Salaam


Toa comment