The House of Favourite Newspapers

Tambwe: Huyu Kamusoko nyie acheni tu!

0

AmissTambwe2Khadija Mngwai na Mohammed Mdose
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, amemtabiria mambo makubwa kiungo wa timu hiyo, Thabani Kamusoko, raia wa Zimbabwe, kuwa atakuwa mchezaji muhimu zaidi siku zijazo katika kikosi hicho.

Yanga imepata ushindi katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo Kamusoko alipiga pasi 121 katika mechi hizo zote, kati ya hizo zilizopotea ni 13 tu na kuonyesha uwezo wa juu katika kukaba.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe alisema: “Kamusoko ni mchezaji mzuri, muda unavyozidi kusonga mbele ndivyo tunavyoweza kuelewana zaidi katika timu, naamini baada ya mechi kadhaa timu itatisha kutokana na kila mmoja kumjua mwenzake, hivyo tutakuwa na timu ya ushindani.”

Mbali na kupiga pasi na kukaba, mchezaji huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kuzunguka uwanjani bila kuchoka, jambo ambalo limemfanya kuwa ‘injini’ muhimu kwenye idara ya kiungo ya timu hiyo.

Leave A Reply