Tambwe: Kwa Yanga Hii Ningefunga Sana

KINARA wa mabao kwenye ligi ya Championship, Amis Tambwe amesema kuwa kwa Yanga hii ya sasa ilivyokuwa tamu yeye angefunga mabao anavyotaka.

 

Tambwe ambaye alicheza Yanga kwa mafanikio makubwa kwa misimu kadhaa nyuma alisema Yanga ya sasa inacheza vizuri na hata washambuliaji wake wapo bora ila kwake Ingekuwa tofauti kidogo.

 

Akizungumza na Championi, Tambwe alisema: “Yanga wana timu nzuri sana na wanacheza vizuri naamini kama mimi ningekuwepo basi ingekuwa balaa pale mbele kwa sababu kuna kitu cha utofauti nakiona.

 

“Nashukuru Mungu kwa sasa nipo DTB nipo na wenzangu tunapambana kuipandisha timu ligi kuu.”

 

Tambwe amefunga magoli sita kwenye michezo minne ya Championship, huku mchezo mmoja akifunga ‘hat-trick’ na juzi Jumamosi walikuwa na kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo na kumalizika kwa suluhu.

 

“Uwa natazama mechi ya Simba na Yanga kama ambavyo imekuwa desturi ya Watanzania wengi.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment