The House of Favourite Newspapers

Tambwe, Ngoma wawekewa kikao Rwanda

0

AMISSI TAMBWE-001Mshambuliaji wa Yanga Mrundi, Amissi Tambwe.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
WAKATI Yanga ikitarajia kucheza na Azam FC, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, safu ya ulinzi ya APR ya nchini Rwanda inayoongozwa na nahodha wake, Albert Ngabo, imeweka mikakati mizito ya kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ili wasitibue mipango yao.

donald-ngoma-yanga_mqjc36fbxrqu1k9l2138qyhm3Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

APR inayomilikiwa na Jeshi la Rwanda, Machi 11, mwaka huu inatarajia kuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuwaondoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa mabao 4-1 huku Yanga wakiwaondoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0.
Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka jijini Kigali, Rwanda, nahodha wa timu hiyo ambaye ni beki wa kushoto, Albert Ngabo, alisema kwa sasa wapo katika maandalizi makali ya kuelekea katika mchezo huo ikiwa na kuhakikisha washambuliaji wa Yanga, Ngoma na Tambwe hawapati nafasi ya kuwafunga kwa kushirikiana na mabeki wenzake.
“Yanga ni timu nzuri sana, ina wachezaji wazuri kama Haruna Niyonzima, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini hata sisi tuna timu nzuri ambayo ina wachezaji wengi vijana, ingawa kwa upande mwingine naamini tutakuwa na kazi kubwa ya kutibua mipango.
“Hofu yangu ipo kwa Tambwe na Ngoma ambao tuliwaona katika mashindano ya Kagame, mwaka jana huko Tanzania, kwa sababu Tambwe ni mzuri kufunga akicheza namba tisa ila Ngoma ana nguvu na kasi kubwa,” alisema Ngabo.

Leave A Reply