Tambwe: Zahera mpe unahodha Yondani

Beki wa Yanga, Kelvin Yondani kushoto akiwa na mchezaji mwenzake Thaban Kamusoko

AMISSI Tambwe amepaza sauti kutoka Burundi hadi Tanzania akimtaka Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amrudishie kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani.

 

Yondani alipewa kitambaa cha unahodha kwenye mechi za maandalizi za msimu uliopita baada ya beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu lakini baadaye Yondani alivuliwa kwa madai ya utovu wa nidhamu.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema; “Tusubiri tuone kama Zahera atakubali ushauri kuhusu hili la kumrudishia Yondani kitambaa japokuwa nafahamu ana misimamo yake na kila mtu anaijua, hakuna mchezaji anayestahili kuwa nahodha zaidi ya Yondani.”

 

“Kwanza kabisa ni mchezaji mzoefu lakini pia kwa sasa ndiye mchezaji mkongwe katika kikosi hicho kuliko wengine wote na ana heshimika na kila mchezaji kutokana na uwezo wake uwanjani.”

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment