Mheshimiwa wa (Tamisemi) Waziri Simbachawene Akioungea na Waaandishi wa habari.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene, leo ameruhusu wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji kuendelea kutumia mihuri ya serikali kama zamani wakati serikali inaendelea kutafuta namna sahihi watakavyoitumia mihuri hiyo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari aliposisitiza kuwa serikali inatambua kuwa viongozi wa serikali za mitaa ndiyo nguzo za utendaji wa serikali na kwamba serikali ilikuwa haikuzuia kutumia mihuri hiyo bali ilikuwa imesitisha kutokana na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa kutokuwa waaminifu kwa kusainisha mikataba mikubwa ya ardhi tofauti na sheria inavyosema.
“Lengo la serikali ni kuwataka wenyeviti waitumie mihuri hiyo vizuri kwani wengi wao wamekuwa siyo waaminifu kwa kuwasainisha watu mikataba mikubwa inayoleta migogoro miongoni mwa wananchi.
“Nawaomba waelewe kuwa hata rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hana mhuri, mwenye mhuri ni katibu mkuu kiongozi, kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wote nao hawana mihuri maana kuna idara husika zinazostahili kuwa na mihuri, hivyo na wenyeviti waliostahili kuwa na mihuri ni watendaji wa serikali za mitaa au vijiji,’’ alisema.
Mkutano huo na wanahabari pia ulihudhuriwa na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa ambao kabla ya tamko hilo walikuwa wamepanga kwenda mahakamani kwa ajili ya kufungua kesi juu ya kutafuta vifungu vinavyowakataza kutokutumia mihuri hiyo.
Kwa habari kamili tembelea www.globaltvtz.com
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.