TAMWA Yawanoa Waandishi Kuhusu Kuripoti Habari za Magonjwa ya Mlipuko
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Taasisi ya AVAC, leo Agosti 17, 2023 kimewakutanisha pamoja waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali katika semina ya namna nzuri ya kuandika na kuripoti habari za magonjwa ya milipuko.
Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Seashell, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben ni miongoni mwa waliotoa mada katika semina hiyo.
Semina hiyo inayofahamika kama ‘Media Science Cafe’ imekuwa jukwaa muhimu la kuwajengea waandishi wa habari uwezo mkubwa wa namna bora ya kuripoti kwa weledi habari mbalimbali za afya hususani magonjwa ya milipuko.
TAMWA na AVAC wamekuwa daraja zuri la uhusiano wa karibu kati ya wanahabari, jamii, wadau wa sekta za afya pamoja na watunga sheria ili kuwa na mrengo wenye uzani sawa katika uwasilishaji wa taarifa hizo kwa manufaa mapana ya jamii.