TANASHA AANIKA SIRI NZITO ZA DIAMOND CHUMBANI

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Tanasha Donna Oketch

DAR ES SALAAM: Mwishoni mwa mwaka jana, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikiri hadharani kuwa; “Tanasha ananijulia kitandani!”  Mapema wiki hii ilikuwa ni zamu ya mpenzi huyo wa Diamond, Tanasha Donna Oketch, raia wa Kenya kuanika siri nzito ya jamaa huyo wanapokuwa chumbani.

 

Katika mahojiano na redio moja nchini Kenya, Tanasha aliulizwa juu ya namna anavyofurahia uhusiano wake anapokuwa chumbani na Diamond ndipo akafunguka bila kigugumizi. Bila aibu, Tanasha alieleza staili ambayo Diamond huwa anapendelea akiwa naye chumbani.

 

Mwanadada huyo ambaye ni mtangazaji wa redio kutoka Mombasa alieleza namna ambavyo humfurahia Diamond hasa anapokuwa kwenye staili anayoipenda (haliandikiki gazetini). Kwa mujibu wa wachambuzi wa penzi la Diamond na Tanasha, wawili hao kila mmoja anamkubali mwenzake kwani kila mmoja amekuwa akimsifia mwenzake.

Kwa mujibu wa Diamond, alishapita na warembo kibao kama Wema Sepetu, Hamisa Mobeto, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na wengine, lakini kwa Tanasha amefika. Wawili hao wamekuwa wakioneshana mapenzi ya njiwa ya kushikana mikono na kubusiana kila baada ya dakika kadhaa wanapokuwa pamoja hasa kwenye mitoko yao.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA


Loading...

Toa comment