The House of Favourite Newspapers

Tanasha Anyang’anywa Gari Kimafia

0

WAKATI Tanasha Donnah akidaiwa kujipanga kumburuza mzazi mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond au Mondi’ mahakamani kudai mali walizochuma pamoja, habari zimevuja kuwa mwanamke huyo amezimwa gari lake kimafya.

 

Amani mtandaoni limedokezwa kuwa gari lenyewe si jingine ni lile alilozawadiwa na Mondi kwenye bethidei yake Julai 7, mwaka jana.

 

Awali uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu ulibaini kuwa, tangu Tanasha ajimuvuzishe kwao nchini Kenya kwa kile kinachodaiwa kuwa amepigwa kibuti na Mondi, gari hilo aina ya Landcruser Prado limepaki nyumbani kwa mama Mondi, Sanura Kassim, eneo la Madale jijini Dar es Salaam.

 

Kutokana na hilo mwandishi wetu alitafuta ubuyu kuhusu gari hilo kwa nini hakuondoka nalo Tanasha ambapo alikutana na maneno haya mazito:

 

“Aende nalo Kenya (Tanasha) kwani ni gari lake,” chanzo cha karibu na familia ya Mondi kilimwambia mwandishi wetu.

Aidha, udadisi zaidi ulipofanywa na mwandishi uliishia kwenye kauli nyingine moto zaidi kwamba:

“Ni kweli alipewa kama zawadi kwenye siku yake ya kuzaliwa lakini kadi ya gari haikuandikwa jina lake,” chanzo kilifunguka.

 

Majibu hayo maana yake ni kwamba uhalali wa Tanasha kumiliki gari hilo umepungua nguvu kutokana na ukweli kwamba jina lililopo kwenye kadi ya gari limedaiwa kuwa ni la ‘mama mzaa chema’ yaani Sanura.

Mama Diamond alipotafutwa ili azungumzie madai ya ‘kumwingiza chaka’ Tanasha kwa kumzawadia gari lisilokuwa na kadi yenye jina lake, alipatikana kwa njia ya simu lakini hakufafanua chochote, badala yake baada ya kusikiliza maelezo alikata simu.

 

Mondi kwa upande wake hakupatikana kwa njia yoyote kutokana na kile kinachotajwa kuwa yuko nje ya nchi kikazi.

 

Mwaka jana katika sherehe ya kuzaliwa Tanasha, Mondi alijimwambafai kwa kutoa zawadi ya magari mawili yenye thamani ya shilingi milioni 160 kila moja ambapo moja alimpatia zawadi mzazi mwenzake huyo na jingine akimpa mama yake mzazi.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Leave A Reply