The House of Favourite Newspapers

TANASHA ATAKIWA KUJIHESHIMU KWENYE MAVAZI

KAMA kawaida wiki iliyopita kwenye safu hii pendwa tulimuweka mtangazaji wa Radio NRG nchini Kenya ambaye pia mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ambaye hivi karibuni aligeuka gumzo baada ya kuvaa gauni lililomuacha wazi sehemu kubwa ya kifua chake hivyo kusababisha matiti kuonekana.

 

Wasomaji wengi wa safu hii walituma maoni yao kuhusiana na hilo ambayo baadhi yanasomeka kama yafuatavyo;

Ni vyema Tanasha akajiheshimu kwani ukivua nguo ya kujiheshimu mbele za watu utapungua wapi jamani, stara ni muhimu kwa mwanamke jisitiri. Aziza Shechambo- Korogwe.

 

***

Vazi alilovaa Tanasha siyo sawa kwa maadili ya Kitanzania kwenye mkusanyiko wa watu akiwa na mpenzi wake, wakati mwingine asirudie tena anatakiwa aulize mila na desturi za waislamu pengine hazijui. Tamba Boy-Sumbawanga.

***

Mimi namlaumu Mondi kwa vile alitakiwa amwelimishe Tanasha mavazi yanayotakiwa kuvaliwa huku ni ya heshima kwani athari za mavazi anayovaa yanaweza kumletea madhara ya kubakwa kwani huku Tanzania siyo kama kwao. Mama Tresha-Dar.

 

***

Pole sana Tanasha hayo mavazi unayovaa mbele za watu ungejua kama unajiaibisha tu hakuna anayependa hata kidogo ndiyo maana hata mashabiki hatukukubali kwa Mondi kwa sababu hujitambui bado dada yangu. Bether- Iringa.

***

Wanawake wa siku hizi wanashindwa kuolewa sababu wanashidwa kujistiri kimavazi kama Tanasha, mavazi yale sijui anatangaza biashara ya kuuza mwili yaani wanawake wa siku hizi wamepoteza ladha ya mapenzi kwani vitu ambavyo mwanaume anatakiwa avione chumbani wao wanavionyesha hadharani. Muddy Madiley-Dar.

 

***

Huyo Tanasha Donna aache wenge hana hata haya mwanamke kwenda kuwakalia maostadhi utupu atakuwa amelaaniwa si bure ndiyo maana tangu aanze mapenzi na Diamond kila siku ni matatizo tu kwa msanii huyo mara kaanguka jukwaani, mara kafungiwa, huyo ana nyota ya kunguni. Jack- Mwanza.

 

***

Dah! Si mchezo, simlaumu huyu binti kwani tamaduni za kwao na mila zao ni sawa tu kutembea kama wanyama hawaoni shida, naona Mondi angemwelimisha mdada wa watu kuhusu mavazi gani avae akiwa huku tusimlaumu jamani wa kumlaumu ni Diamond maana alitakiwa ampe darasa. Mama Beaty-Malindi.

***

Huyu Tanasha kwanza ajue kabisa anamshushia hadhi Mondi, tena mbele ya shehe mkuu, ina maana alikuwa hajui anakokwenda kuna viongozi? Ushauri wangu ni kwamba ajiheshimu mwenyewe na awe anaangalia nguo anazovaa ziwe zinaendana na sehemu anayokwenda na siyo kuvaavaa nguo zinazomwonyesha mwili wake kila mahali. Mourine Cassian-Iringa.

 

WIKI hii tunamleta kwenu mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye hivi karibuni alitoa kauli kwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwa hatokuja kuimba tena baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo.

 

Baada ya Dimpoz kupona na kuachia wimbo, mchekeshaji huyo ameandamwa mitandaoni kuhusiana na kauli yake aliyoitoa hivyo kutumia ukurasa wake wa Instagram kuomba radhi.

Mpenzi msomaji, nini maoni yako kwa Steve Nyerere juu ya kauli yake?

 USIPOJIPANGA TUNAKUPANGA | RISASI MCHANGANYIKO

 

 

Kilichomuua GODZILLA, Dada Asimulia “Aliona Watu Wanamfata”

Comments are closed.