Tanasha Atibua Saumu za Watu

DAR: Baada ya kubadili dini kutoka Ukristo na kuwa Muislam, mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’, Tanasha Donna ambaye kwa sasa anaitwa Aisha Donna, ametibua saumu za watu kwa kushindwa kujisitiri kama mwanamke wa Kiislam hasa katika mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 

Kabla ya tukio hilo, wikiendi iliyopita, Tanasha na rafiki yake wa karibu, Jamal Gaddafi walifuturisha kwa mara ya kwanza, wakiwa na rafiki zao kuashiria kwamba wamefunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 

Kwa baadhi ya mashabiki wake nchini Kenya, ilikuwa ni mara yao ya kwanza kujua kwamba, Tanasha kwa sasa ni Muislam.

 

Gazeti la IJUMAA linafahamu kwamba, Tanasha alibadili dini mwaka jana mwishoni alipokuwa mkoani Kigoma kwa ajili ya shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya muziki ya Mondi.

 

Baada ya tukio hilo la kufuturisha, siku mbili baadaye, Tanasha alitupia picha mtandaoni zikimuonesha maungo nyeti huku akishindwa kujisitiri kama mwanamke wa Kiislam.

 

Hata hivyo, wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook hawakushangazwa na kujua kwamba amebadili dini, bali walishangazwa na uvaaji wake ambao hakuendana na stara ya mwanamke wa Kiislam.

 

Wengi walisema kuwa, walichukizwa na mavazi ya Tanasha kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani huko ni kuwatibulia wenzake saumu zao.

 

Wengine walikwenda mbele zaidi na kusema kuwa, Tanasha hastahili kulaumiwa bali anahitaji kufundishwa kuwa Uislam unahitaji ustaarabu mno linapokuja suala la kujisitiri kimavazi na hasa katika mfungo kama huu.

 

Katika mahojiano maalum, mapema wiki hii, kwa mara ya kwanza, Mondi alithibitisha Tanasha kubadili dini kwa ajili ya kufunga ndoa, lakini mambo hayakwenda sawa.

Stori: IMELDA MTEMA, Ijumaa


Loading...

Toa comment