Tanasha Awajia Juu Waliomtusi!

Dar: Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch amewajia juu mashabiki waliomtusi baada ya kuomba pesa kwa ajili ya kutengeneza video fupi za nyimbo maalum za wapendwa.

 

Tanasha aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuwaambia mashabiki kutoa pesa shilingi elfu moja ya Kenya, kwa ajili ya kutengenezewa video fupi za wapendwa wao kama ni mama, baba au hata mpenzi ambapo wengi walitoa mapovu kama yote.

 

“Kwa nini tulipe pesa kwa kutengeneza kitu kifupi kama hicho, sisi ni mashabiki wako ambao tunakufanya ujulikane kwani huwezi kufanya kwa upendo…’’

 

Aliandika shabiki mmoja. Kufuatia hali hiyo, Tanasha aliwajia juu na kuwaambia hakuna kitu cha bure hivyo wasimfikirie vibaya kwani kufanya vile ni kama kulipia kumuona msanii au kununua bidhaa.

 

“Mashabiki wasinifikirie vibaya, kulipia video ni kama vile unavyokwenda kununua bidhaa sokoni au kutoa pesa kwa ajili ya kuingia kwenye shoo ya kumuangalia msanii unayempenda,’’ alijibu Tanasha kwenye Insta Stori kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Stori: Happyness Masunga. Ijumaa

Toa comment