Tanesco Yatoa Neno Kukatika Kwa Umeme
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha Umeme ya Gridi ya Taifa kuanzia majira ya saa 8:22 Usiku hivyo kupelekea baadhi ya maeneo nchini kukosa huduma ya umeme.
Wataalam wa shirika hilo wanafanya jitihada kutatua changamoto hiyo ili kurudi kwa huduma ya Umeme maeneo inayopokosekana.