The House of Favourite Newspapers

Tanga Cement Yanyakua Tena Tuzo Za NBAA

0
Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager (kulia), akiwa katikapicha ya pamoja na Maofisa wengine wa kampuni hiyo wakiwa wameshika Tuzo walizoshinda katika hafla ya utoaji tuzo wa Uwaandaaji na Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (kushoto), akikabidhi Tuzo kwa Meneja Mauzo kitaifa wa Kampuni ya Tanga Cement Mhandisi Leslie Masawe wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ambapo Tanga Cement ilishiriki kwenye maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam Novemba 30, 2022
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Jamal Kassim Ali akikabidhi tuzo ya Mshindi wa kwanza kipengele cha wazalishaji viwandani katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 kwa Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager .

 

Baadhi ya Maofisa kutoka Tanga Cement wakiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Washindi wa jumla wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Leave A Reply