The House of Favourite Newspapers

Tangawizi, Iliki, Mdalasini kwa Kulinogesha Penzi Lako!

LEO kwenye safu hii ya watu wazima tutaona jinsi ya kumfanya mpenzi awe karibu yako kwa kutumia mzizi wa tangawizi, mdalasini na sukari.

Vitu unavyohitaji:

Maji ya rose

Vijiko 17 vya sukari

Kijiko 1 cha mzizi wa tangawizi iliyosagwa

Kijiko 1 cha mdalasini uliosagwa.

Kijiko kimoja cha mbegu za iliki.

Kila kiungo kina nia yake, changanya vyote kwenye kijagi kidogo, baada ya hapo funika kisha funga na ribbon ya njano, weka chumbani sehemu ambayo ni salama, wakati unafunga sema maneno haya; ‘namtuliza laazizi wangu, tusikilizane, tupendane kama sukari na viungo hivi vyote vinavyopendwa na watu.

Maji ya rose ni kwa ajili ya kulikoleza penzi, tangawizi itamfanya awe na hamu na wewe na mdalasini na iliki kwa ajili ya kulilinda penzi lako kwa uaminifu.

Comments are closed.