Tangazo Muhimu Kutoka Sekretarieti Ya Ajira

ANGAZO MUHIMU TOKA SEKRETARIETI YA AJIRA
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Katibu wa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwaatarifu waombaji kazi wa kada za “Geologist” II na “Engineer” II (Mineral Processing) zilizotangazwa kwa niaba ya Tume ya Madini Tanzania (TMC) kuwa kada ya “Geologist” II itafanya usaili wa Mchujo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) mnamo tarehe 18/10/2019 saa 3:00 Asubuhi katika Ukumbi wa LECTURE THEATRE C na tarehe ya usaili wa Mahojiano ni tarehe 21/10/2019 saa 1:00 Asubuhi Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jengo la Utumishi Kivukoni.

Aidha kada ya “Engineer” II (Mineral Processing) haitakuwa na usaili wa Mchujo na usaili wa Mahojiano utafanyika tarehe 21/10/2019 saa 1:00 Asubuhi Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jengo la Utumishi Kivukoni.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
15/10/2019

👉 Bonyeza hapo chini kuendelea kupata matangazo mbalimbali ya Ajira,Nafasai za Kazi

Toa comment