The House of Favourite Newspapers

Tango na baking soda kwa wenye UTI

0

tango.jpegLeo kwenye safu hii tutaongelea tango linavyoweza kukusaidia kutopata ugonjwa wa UTI kwani linafanya kazi kama maji mwilini.

Kama wewe si mnywaji wa maji na unapatwa na ugonjwa huo mara kwa mara nakushauri kula tango moja kila siku kwa ajili ya ulinzi wa mwili wako.

Kunywa baking soda

Baking Soda imekuwa ikisaidia kwa mambo mengi hasa magonjwa, mfano tumewahi kuiandika kwa kuzuia kiungulia, kung’arisha meno na magonjwa mengine.

Kwa upande wa UTI, baking soda imekuwa ikisaidia kupunguza asidi kwenye mkojo hivyo kama una ugonjwa huu, unashauriwa kunywa ili kupunguza makali yake na hata kuponya moja kwa moja

Jinsi ya kutumia kama dawa

– Chukua kijiko 1 cha chai cha baking soda.

– Glasi moja ya maji

Ukishapata vyote, koroga kwenye maji safi kisha kunywa glasi nzima. Kunywa kinywaji hiki asubuhi na mapema kabla ya kula kitu, usitumie tiba hii zaidi ya wiki moja.

Kumbuka: Usiache kwenda haja ndogo kila unapojisikia kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maumivu, kama una tabia ya kubana mkojo ni mbaya ukiwa na ugonjwa huu kwa sababu itakuongezea maambukizi.

Leave A Reply