The House of Favourite Newspapers

Tani za Kutisha za Cocaine Zaingizwa Kupitia Sukari

0

madawayakulevyaPicha ya madawa ya kulevya (na maktaba).

Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM! Serikali imetahadharishwa kuhusu madai kwamba, nyuma ya pazia ya uingizwaji wa sukari kutoka nje kwenye nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kuna tani za kutisha za usafirishaji wa madawa ya kuleva ‘unga’ aina ya cocaine na heroin, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wafanyabiashara katika nchi hizo wamekuwa wakitumia mwanya wa kuagiza sukari toka nchi zinazozalisha kwa wingi bidhaa hiyo, kuambatanisha na unga na kuingiza kwenye nchi zao.

Magufuli amalizia Baraza la Mawaziri-001Rais Dk. John Pombe Magufuli

“Hili napenda kuwawekea wazi kwamba, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, baadhi lakini siyo wote, kutoka nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wamekuwa wakitumia nafasi ya kuagiza sukari toka nchi kama Brazil, India, China na Thailand kusafirisha na madawa ya kulevya kwa siri bila serikali husika kujua.

“Mfano, mtu anaagiza sukari mifuko laki mbili lakini kati ya hiyo, mifuko laki moja na elfu themanini ni sukari lakini mifuko ishirini ni madawa ya kulevya.

“Mfanyabiashara anakuwa anaijua mifuko yenye madawa ya kulevya kwa sababu imewekwa alama kwa mawasiliano na watu wake. Inapofika bandarini au kwenye ghala lake anaitoa na kuiingiza sokoni.

????????????????????????????????????Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga. (Mahojiano na Kitwanga yalifanyika wakati bado akiwa waziri, kabla ya Rais John Magufuli kutenguliwa uteuzi wake jana).

“Ndiyo maana utakuta sukari ya nje inauzwa kwa bei ya chini kuliko inayozalishwa kwenye nchi husika kwa sababu, faida ya ule unga mifuko ishirini ukiuzwa, inashinda faida ya ile mifuko laki moja na elfu themanini ya sukari. Kwa hiyo ndiyo maana baadhi ya nchi za ukanda huu zimekuwa vituo vikuu vya biashara ya unga duniani.

Sukari-001“Njia hii ilibuniwa baada ya ile njia ya zamani ya kusafirisha unga kwa kuuweka ndani ya matairi ya magari au kwenye chasesi za magari kugundulika,” kilisema chanzo hicho.

“Lakini pia njia nyingine ambayo baadhi ya wafanyabiashara wanatumia kusafirisha unga ni usafirishaji wa saruji (cement) toka nchi zinazozalisha, kama vile China, India, Iran, Indonesia nakadhalika.

 “Njia ni ileile, baadhi ya mifuko inakuwa na unga ndani badala ya saruji. Hii huwashinda hata wale vibarua wanaopakua mifuko kwenye usafiri mmoja kwenda mwingine kubaini kama mfuko alioubeba ndani yake kuna unga badala ya saruji au sukari,” kilisema chanzo.meli ya mizigo1

Meli ya Mizigo.

Chanzo kilizidi kuweka wazi kwamba, baadhi ya nchi, anapotokea kiongozi wa juu kuwa mkamataji wa wauza unga, wafanyabiashara hao huweka mikakati ya makusudi ili ikiwezekana kiongozi huyo aondoke kwenye nafasi hiyo.

“Baadhi ya nchi zinawatumia hata wanasiasa kufanya njama za kuwaondoa madarakani viongozi wanaopambana na wauza unga ili biashara yao isikwame. Hii imetokea hata kwenye baadhi ya nchi kubwa duniani,” kilisema chanzo.

sacp mihayoKamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Mihayo.

TANZANIA IKOJE?

Ili kujua kama hali hiyo imewahi kutokea nchini, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Mihayo Msikhela ambapo baada ya kumsomea madai hayo, alisema:

“Hilo naweza kusema ndiyo nalisikia kwako, lakini nakuahidi kuanza kulifuatilia kwa kina ili kujua kama lipo lichukuliwe hatua za kupambana nao.”

Baada ya kuzungumza na kamanda huyo, pia gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga (kabla hajaachishwa kazi) ambaye mahojiano yake na paparazi wetu yalikuwa hivi:

Risasi Jumamosi: (baada ya kujitambulisha) mheshimiwa kuna taarifa kuhusu sukari kwamba…

Waziri: Ahaa! Sitaki kuzungumzia mambo ya politics (siasa).

Risasi Jumamosi: Mheshimiwa naomba unisikilize kwanza…

Waziri: No! No! No! Hayo mambo ya wanasiasa waulizeni wanasiasa wenyewe. Mimi niambie kuna mtu gani aliye chini yangu, amefanya kosa ili nimtimue, siyo hayo mambo ya siasa.

Risasi Jumamosi: Lakini mkuu nilikuwa nataka kukupa taarifa za ishu ya madawa ya kulevya…

Waziri: Sikia bwana! Mimi unipe masuala ya fact (jambo ambalo limetendeka) siyo taarifa.

Risasi Jumamosi: Oke, basi nakushukuru mheshimiwa.

Waziri: Next time (wakati mwingine) unipigie ukiwa na fact siyo taarifa. Mimi nataka mambo ya kazi tu!

Mpaka waziri huyo anamaliza kuzungumza na Risasi Jumamosi hakuwa amejua alichotakiwa kukijua ili akiendee mbele kwa uchunguzi licha ya wakati fulani, Rais Magufuli alisema amekuwa akivitumia vyombo vya habari, yakiwemo magazeti (kama hili la Risasi Jumamosi), kupata taarifa mbalimbali.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply