The House of Favourite Newspapers

TanTrade Yapendekeza Mkataba wa Ruzuku za Uvuvi wa WTO Uzingatie Wafanyabiashara, Wavuvi Wadogowadogowadogo

0
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Biashara TanTrade Bw. Freddy Liundi akiambatana na Afisa Biashara Mwandamizi Bi. Magreth Shirima, Afisa Habari Norah Thomas na Daniel Joseph ambapo Bw.Liundi amesema hayo katika Warsha ilioandaliwa na Shirika la Biashara Duniani (WTO) wenye lengo la kujenga uelewa kuhusu Mkataba wa kudhibiti ruzuku kwenye sekta ya uvuvi (WTO Fisheries Subsidies Agreement) inayofanyika kuanzia tarehe 2-5 Mei 2023 jijini Dar es Salaam ikihusisha washiriki kutoka nchi za Afrika zinazoongea Kiingereza ikiwa ni pamoja na South Afrika, Kenya, Uganda, Lesotho na Misri
 Bw. Liundi amesema TanTrade inapongeza jitihada zinazofanywa na Shirika la Biashara Duniani (WTO) katika kutunza rasimali za Bahari na inaendelea kushirikiana nalo katika kutoa ushauri wa kisera unaozingatia ustawi wa Wafanyabiashara na Wavuvi wadogogo nchini.
Mkataba wa Kudhibiti Ruzuku Sekta ya Uvuvi umejadiliwa takribani miaka 20 kabla ya nchi wanachama wa WTO kufikia  makubaliano ya awali mwezi Juni 2022 wakati wa Mkutano wa 12 wa WTO wa Mawaziri unaofahamika kama Twelfth Ministerial Conference -MC12 wenye lengo la kulinda uendelevu wa rasilimali hai zilizoko baharini hususan samaki kupitia kudhibiti ruzuku ambazo zinapelekea wavuvi kuwa na uwezo mkubwa wa kuzunguka bahari zote na kufanya uvivi usio endelevu kwa kuvua kupita kiwango.
Warsha hiyo imefunguliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar Bw. Khamis  Mwalimu ambapo ameseama ni muhimu mkataba huo kutoa nafasi ya kisera kwa nchi zinazoendelea kwa kuzipatia upendeleo maalum ili Serikali ziweze kuendeleza Sekta ya Uvuvi na rasilimali hai zilizoko baharini.
Bw. Mwalimu amesema kuwa sekta ya uvuvi inamchango mkubwa kwa uchumi wa bara la Afrika ambapo kwa Tanzania ina kilometa 223 za eneo la uvuvi katika bahari ya hindi na kutoa ajira, hifadhi ya chakula, kipato kwa watu na Serikali hivyo ni muhimu mkataba huo kuizingatia mahitaji hayo.
Awamu ya pili ya majadiliano ya kuhitimisha mkataba huo yanaendelea WTO ambapo masuala muhimu yanayotarajiwa ni pamoja na kuhakikisha Mkataba huo unajumuisha upendeleo  maalum kwa nchi zinazoendelea na wavuvi wadogo (artisanal fishing) na yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mkutano wa 13 wa WTO wa Mawaziri (MC13) utakaofanyika Fenruari 2024.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa WTO Bi. Angella Ellard ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuandaa warsha hiyo na kwa ushirikiano mzuri na
kusema kuwa warsa hiyo ni muhimu ya kwakuwa bahari inakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa idadi ya samaki ambayo inaendelea bila kusita. Aliangazia kwamba serikali nyingi zinaendelea kutoa ruzuku za uvuvi bila kuzingatia athari zake kwa ustahimilivu. Ruzuku hizo zinakadiriwa kufikia dola bilioni 35 kwa mwaka kote ulimwenguni, ambapo dola bilioni 22 zinahusiana na kuongeza uwezo wa uvuvi. Ruzuku hizo zinafanya meli nyingi za uvuvi kufanya kazi kwa muda mrefu na mbali zaidi baharini kupelekea athari kwa mazingira na lasilimali za bahari.
Leave A Reply