The House of Favourite Newspapers
gunners X

Tanzania Kuanza Kuzalisha “Smart Phone”

0

Serikali imemtaka muwekezaji wa kiwanda cha Raddy Fiber chenye uwezo wa kuzalisha nyaya za mkongo a mawasiliano kuharakisha ujenzi uliosalia ili kuwezesha malengo ya Serikali ya kuanza uzalishaji wa simu janja ifikapo mwezi Juni 2022.

 

Hayo yamebainishwa na Rais Samia wakati akizindua kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mapema Desemba 03, 2021 na kusema kuwa Serikali imejipanga kutekeleza uzalishaji huo kwani madini yanayotumikakuzalisha vifaa vya simu hizo yanapatikana nchini.

 

“Tunategemea kuanza uunganishaji wa simujanja ifikapo mwezi June, 2022 ili kuwezesha nchi yetu kuzalisha simu hizi na bahati nzuri tuna madini ambayo kesho kutwa tunakwenda kusaini na makampuni ili tuanze mchakato huo.”

 

Rais Samia amemtaka Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hassan Ramadhani Mlanzi kuhakikisha kuwa ifikapo mwakani wawe wamekalimilisha ujenzi wote wa kiwanda hicho cha kwanza ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, cha tatu kwa Afrika nzima pindi kitakapokamilika kwani kwasasa ni cha nne kwa Afrika yote.

Leave A Reply