The House of Favourite Newspapers

Tanzania Moja wafurahishwa na mapokezi Global

Huu ni mtandao wa Vijana wanaoamini katika kutafuta fursa za vijana na Ushiriki wao wa Moja Kwa Moja kwenye Jitihada za maendeleo nchini bila kujali tofauti zao za dini, Itikadi, chama au ukabila, Tanzania Moja wamefurahishwa na mapokezi ya Global.


Tanzania Moja Movement inayoendesha shughuli zake kwa kujitolea kupitia warsha, semina, makongamano na uhamasishaji mbalimbali yanayolenga kuwakutanisha vijana na wadau wakubwa wa maendeleo kwa upande wa Serikali na sekta binafsi walitembelea Ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar.


Wakizungumzia umoja wao wa Tanzania Moja, walisema itajiendesha kupitia michango ya wanachama wake na kwa kupitia wadau mbalimbali wanaounga mkono.
“Kiufupi, utayari wa kujitolea ndiyo msingi mkuu wa rasilimali zote zitakazopatikana kwenye kuendesha shughuli zetu.


“Tanzania Moja inataka kuona Vijana wengi iwezekanavyo wamezingatiwa kwenye jitihada za maendeleo zinazoendelea ikiwemo Miradi Mikubwa inayotekelezwa na Serikali kama Ujenzi wa Reli ya Kisasa na Stiegler’s Gorge. Lakini pia kuhamasisha Ushiriki wa Moja Kwa Moja wa Vijana kwenye kuwania nafasi za uongozi na utendaji Serikalini na kwenye Sekta Binafsi ili iwe rahisi kupambania maslahi ya vijana wenzao,” alisema mmoja wa viongozi wao.

Comments are closed.