The House of Favourite Newspapers

Tanzania na China kuendelea kudumisha ushirikiano

0

Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia), Bw. Clement Mshana pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili (wa pili kulia) wakifurahia zawadi za vitambaa vilivyonakshiwa na wabunifu wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015.

 Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kilichochongwa na wasanii wa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago.

Hapa ni furaha tupu katika uzinduzi huo.

Waigizaji wa filamu ya’The Young Doctor’ Zhang Yi na Zhou Fang wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.

Leave A Reply