Tanzania na Msumbiji Zatia Saini Mikataba ya Ulinzi na Usalama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kabla ya kuanza mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Ikulu ya Maputo tarehe 21 Septemba, 2022.

Msumbiji na Tanzania Septemba 21, 2022 zimesaini mikataba miwili ya ushirikiano mjini Maputo inayolenga kupambana na ugaidi na uhalifu.

Msumbiji kwa sasa inapambana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa Cabo Delgado nchini humo.

 

Mikataba hiyo ilisainiwa ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya siku tatu ambayo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anafanya nchini Msumbiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Ikulu ya Maputo  tarehe 21 Septemba, 2022.

”Katika kuhakikisha tunapambana na magaidi, kupitia mahusiano haya leo tumeweza kutia saini katika eneo la usalama na ulinzi, na hii ni hatua muhimu sana katika kusonga mbele” amesema rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Mji wa Maputo mara baada ya kutembelea Kituo cha uzalishaji wa Nishati ya Umeme nchini Msumbiji tarehe 21 Septemba, 2022.

Mbali na kupambana na wanajihadi, Rais Filipe Nyusi alisema nchi hizo mbili kwa sasa zimejikita katika unyonyaji wa hidrokaboni ambayo ni nyenzo za ujenzi wa vyanzo muhimu vya nishati kama makaa ya mawe na gesi.

Rais Samia pia alisisitiza haja ya nchi zote mbili kuimarisha usalama kwa sababu ya mpaka wa pamoja wanaoshiriki.

4295
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment