Tanzania Yaipiga Niger Goli 1-0 Ugenini, Mfungaji Charles M’mombwa
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza vizuri Kuwania Kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Niger goli 1-0, mfungaji akiwa ni Charles M’mombwa katika mchezo wa Kundi E
Mtanange huo umepigwa kwenye Uwanja wa Marrakech Nchini Morocco huku Niger ikitambulika kuwa nyumbani baada ya viwanja vyao kutokidhi vigezo vya ubora unaohitajika
Mchezo unaofuata kwa Tanzania ni dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Mkapa mnamo Novemba 21, 2023. Timu nyingine katika kundi hilo ni Zambia na Congo wakati Eritrea ilijitoa kwenye ushiriki.
MSIMAMO KUNDI E
1. 🇿🇲 Zambia (3)
2. 🇹🇿 Tanzania (3)
3. 🇲🇦 Morocco (0)
4. 🇳🇪 Niger (0)
5. 🇨🇬 Congo (0)