Tanzania Yatinga Hatua Ya Makundi, Yaipiga 3-0 Burundi -Kombe la Dunia

Kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichoanza dhidi ya burundi leo.

Hatimaye Tanzania inatinga hatua ya makundi katika kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 kwa ushindi wa penati 3-0 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa marudiano uliomalizika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vita ya magolikipa wawili wa KMC ambao wote wanazitumikia timu zao za Taifa leo zimemalizika kwa mmoja kuibuka mbabe baada ya kuipeleka timu yake hatua ya makundi.

Kikosi cha timu ya Burundi.

Juma Kaseja mlinda mlango wa Tanzania anayekipiga klabu ya KMC na Jonathan Nahimana wa timu ya Taifa ya Burundi ambaye aliingia akichukua nafasi ya Justin Ndikumana dakika ya 119.

 

Kwenye mchezo wa leo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada Kaseja ameokoa penalti moja na mbili wapigaji wa Burundi wamekosa.

 

Kwa upande wa Tanzania mfunguzi alikuwa ni Erasto Nyoni kisha Himid Mao na msumari wa mwisho ukapachikwa na Gadiel Michael.

Tanzania inasonga mbele kwenye hatua ya makundi Kwa Ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilika Kwa kufungana bao 1-1.

 

Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana nguvu Kwa kufungana bao 1-1.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL


Loading...

Toa comment