Tanzanite noma, Yatwaa Ndoo Cosafa

TIMU ya Taifa ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Cosafa kwa kuichapa timu ya Zambia kwa mabao 2-1,katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja Uwanja wa Wolfson,Port Elizabeth,Afrika Kusini.

 

Tanzanite ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Opa Clement aliyefunga dakika ya 24 na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa mbele kwa bao moja.

 

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Zambia kufanikiwa kuchomoa bao dakika ya 55 na kisha Tanzanite kujipatia bao la pili kupitia kwa Protasia Mbunda kwa shuti kali dakika ya 87.Ikumbukwe mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana Zambia walishinda kwa mabao 2-1.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu kutokea Afrika Kusini kocha mkuu wa kikosi hicho Bakari Shime alisema kuwa alijaribu kubadilisha namna ya uchezaji na kuongeza mbinu zaidi za kiuchezaji ikiwemo kushambulia bila kuchoka kitu ambacho wachezaji walikifanyia kazi na hatimaye kupata ushindi.

 

“Nilibadilisha namna ya uchezaji baada ya kugundua udhaifu wa wapinzani wetu, nashukuru wachezaji wangu walifanyia kazi yale tuliyowaagiza na hatimaye tukapata matokeo,” alisema Shime.

Issa Liponda

 


Loading...

Toa comment