The House of Favourite Newspapers
gunners X

TANZIA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Katani Ltd Afariki Dunia

0

MKURUGENZI wa zamani wa Katani Limited, Salum Shamte, amefariki dunia katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu, mkewe Mariamu Shamte amethibitisha. 

 

Alhamisi Oktoba 31, 2019, Shamte ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na wenzake Juma Shamte ambaye ni mkurugenzi wa sasa wa Kampuni hiyo,  na Mjumbe wa Bodi ya Katani, Fatma Diwani, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga wakikabiliwa na mashtaka matatu.

 

Mashtaka hayo ni ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Sh. bil. 1.14 kwa vyama vya msingi vya ushirika (Amcos) ambayo walidaiwa kuyatenda kati ya Januari 2008 na Agosti 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga na Mkoa wa Tanga, walikula njama kutekeleza mpango wa uhalifu.

 

Oktoba 25, 2019 Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) ilimteua Angelina Ngalula kuwa kaimu mwenyekiti wa taasisi hiyo wakati taratibu za kisheria zikiendelea kufanyika dhidi ya  Shamte ambaye siku hiyo alikuwa amefikisha takribani siku 10 polisi.

 

Kwa habari zaidi kuhusu msiba huu, endelea kufuatilia taarifa zetu.

Leave A Reply