The House of Favourite Newspapers

TANZIA: BABA MZAZI WA ALIKIBA AFARIKI DUNIA

Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Mzee Saleh Kiba amefariki Dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mdogo wa Alikiba, Abuu Kiba ambaye amezungumza na globalpublishers.co.tz  amesema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa Muhimbili na msiba upo nyumbani kwao Kariakoo na kwamba mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni katika Makaburi ya Kisutu.

 

Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa.

Inna lillahi wainna ilayhi raji’un. Pole sana kwa familia ya Kiba.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.