Tanzia: Baba wa Mabeste Afariki Dunia

MSANII wa Bongo Flava, William Ngowi, maarufu kwa jina la ‘Mabeste‘ amepata pigo baada ya kuondokewa na baba yake mkubwa ambaye amefariki dunia Jumanne, Januari 12, 2020, mkoani Morogoro.

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mabeste amethibitisha na kuposti picha ya baba yake huyo enzi za uhai wake na kuandika R.I.P Baba.

Mwili wa mzee Ngowi umesafirishwa kwenda Moshi Kilimanjaro kwa maziko jana ambapo anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi, Januari 18, 2020.

 

Global Group tunapenda kutoa pole kwa Mabeste pamoja na familia yake kwa kumpoteza baba yao mzazi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe. Amen!

 

SHOO YA YOUNG LUNYA, MIMI MARS ILIVYOWAINUA MASHABIKI DAR


Loading...

Toa comment