The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Diwani wa Mbagala Kuu Afariki Dunia

0

DIWANI wa Mbagala Kuu Shabani. Othman Abubakari (CCM), amefariki dunia katika moja ya nyumba ya kulala wageni iliyoyopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

 

 

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtimika na kuwa mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Tanita yaliyopo eneo la Kibonde Maji.

 

 

Mmoja wa wahudumu nyumba hiyo ya kulala wageni (jina lake linahifadhiwa) amesema diwani huyo alifika akiwa na gari wakiwa na msichana usiku wa kuamkia juzi na kuchukua moja ya chumba katika nyumba hiyo.

 

 

Amesema asubuhi baada ya kuamka wakati akifanya usafi ndipo alipoukuta ufunguo wa chumba alichokuwa amekichukua diwani huyo na msichana huyo ukiwa umetupwa chini ambapo alishituka na kwenda katika chumba hicho na kukuta kikiwa kimefungwa na kilipofunguliwa walimkuta diwani huyo akiwa amefariki lakini yule msichana waliyekuwa naye hayupo.

 

 

Muhudumu huyo amesema baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na baada ya kuwahoji waliuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 

Leave A Reply