The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Jaji Upendo Msuya Afariki Dunia

0
Upendo Msuya enzi za uhai wake.

 

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye alijiuzulu  hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akithibitisha kifo hicho, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

 

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga

 

Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

 

LIVE: Ziara ya Waziri wa Utumishi, Angellah Kairuki Wilaya za Mkoa wa Dar

Leave A Reply