The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Kamanda wa Polisi wa Zamani Dkt. Mohamed Chico Afariki Dunia

kamanda

Kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Mohamed  Chico amefariki dunia  usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Awadhi Chico, mazishi yake yamepangwa kufanyika leo Jumapili 22/01/2017 jioni katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kijitonyama. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.

Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabiti na ailaze roho yake mahali pema peponi – AMINI

Comments are closed.