The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mama wa Kocha Guardiola Afariki kwa Corona

0

 

 

MAMA wa meneja (kocha) klabu ya Manchester City ya Uingereza,  Pep Guardiola, aitwaye Dolors Sala Carrió,  amefariki dunia mjini Barcelona akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

 

“Washirika wa klabu hiyo wamekuwa  wakituma ujumbe wa rambi rambi katika kipindi hiki kigumu kwa Pep, familia yake na marafiki zake wote ,” umesema ujumbe wa timu ya Manchester City uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Ongezeko la Jumatatu la vifo 637 vya virusi vya corona linamaanisha kuwa hadi sasa watu 13,055 wamekwishakufa nchini Hispania kutokana na janga hilo. Mwezi uliopita, Guardiola alitoa mchango wa euro milioni 1 sawa na pauni 920,000 kwa jili ya kusaidia katika vita dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona.

 

Pesa hizo zitatumika katika kununulia vifaa vya matibabu na kujikinga na maambukizi kwa ajili wahudumu wa tiba wanaowashughulikia wagonjwa waliolazwa hospitalini. Barcelona iko katika jimbo la Catalonia, ambako ni moja ya maeneo nchini Hispania yenye idadi kubwa ya visa vya corona.

 

Manchester United ilituma ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii ikisema klabu hiyo “imesikitishwa sana kusikia taarifa hii mbaya “, na kuongeza kuwa: “Tunatuma rambirambi zetu kwa Pep na familia yake.”

 

Guardiola ambaye ni Mhispania, mwenye umri wa miaka, 49, amekuwa meneja wa Manchester City tangu mwezi Julai 2016 baada ya kuhudumu kama meneja katika timu za Barcelona na Bayern Munich.

 

Leave A Reply