Tanzia: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia

hafidh-mbDODOMA: Mbunge wa Jimbo la Dimani lililopo visiwani Zanzibar, Mhe. Hafidh Ali Tahir (CCM) amefariki dunia saa 9 alfajiri ya leo katika Hospitali ya General iliyopo mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.

Marehemu pia alikuwa mwanamichezo, mwamuzi wa FIFA na mpenzi wa Klabu ya Yanga kindakindaki na ni jana tu alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge Wana-Yanga mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae.

Mhe. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment