Tanzia: Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama TASAC Afariki Dunia
MHANDISI Japhet L. Loisimaye amefariki dunia jana Jumapili, Mei 10, 2020 jioni jijini Dar es Salaam.
Loisimaye alikuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (DMSE) katika Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).


