Tanzia: Mwanamuziki Maarufu DJ Arafat Afariki Dunia

 

MWANAMUZIKI maarufu wa mitindo ya Coupé-Décalé nchini Ivory Coast, Houon Ange Didier ‘DJ Arafat (33), amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongwa na gari, jana Jumatatu, Agosti 12, 2019, jijini Abidjan.

Inaelezwa kuwa, hilo lilitokea majira ya saa tano usiku wa Jumatatu, Agosti 11, wakati nyota huyo wa Cote d’Ivoire DJ Arafat na kundi la marafiki zake walikiwa   safarini  kuelekea Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast.

Mita chache tu baadaye, aligongana uso kwa uso na gari lililokuwa likiendeshwa na mwandishi wa habari wa Radio ya Taifa ya Ivory Coast.

Ajali hiyo ilikuwa mbaya, picha na video ambazo zilirushwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha DJ Arafat akiwa amelala barabarani, amepoteza fahamu ambapo aliwahishwa haraka hospitalini kutibiwa kabla ya kufariki dunia jana Jumatatu majira ya saa 2:10 asubuhi.

 

DJ Arafat atakumbukwa kwa staili yake ya kufoka (rapping), ambapo amewahi kuimba na wasanii wakubwa akiwemo J. Martins.

 

J. Martins featuring Dj Arafat – Touchin Body (Official Video)


Loading...

Toa comment