The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Mzee Jengua Afariki Dunia

0

 

MSANII mkongwe wa michezo ya runingani na filamu za Kibongo, Mohamed Fungafunga almaarufu Mzee Jengua, amefariki leo, Desemba 15, 2020 Mkuranga mkoani Pwani.

 

Msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’, amethibitisha kufariki kwa msanii huyo na kueleza kwamba alikuwa akiugua kwa muda mrefu baada ya kupooza na kwamba alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani kwa mwanaye, Mkuranga.

 

Mzee Jengua alipata umaarufu mkubwa katika mchezo wa runinga wa Kidedea uliokuwa ukirushwa na kituo cha ITV na kutayarishwa na Chemchem Arts Group, akiigiza kama mzee katili na mwenye roho mbaya.

 

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kupooza.

 

Jengua aliigiza kwenyefilamu za Kidedea, Handsome wa Kijiji, Kashinde na zingine nyingi.

 

Mungu aiweke roho yake mahali pema.
Amin!

Leave A Reply