The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Wafanyakazi Wawili TBC Wafariki Dunia

0

IKIWA ni takriban siku kumi tangu kumpoteza nguli na mwandishi fundi wa habari, Marin Hassan Marin, Shirika la Utangazaji la Tanzania limewapoteza manguli wengine wawili ndani ya shirika hilo.

 

Marehemu hao ni Joseph Kambanga (Meneja wa Teknolojia , Habari na Mawasiliano – TEHAMA – pichani kushoto) na Lutengano Haonga (Mwandishi Mwandamizi – pichani kulia).

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ameandika;

“Ni uchungu mkubwa kuwapoteza Joseph Kambanga “Jenerali” (Meneja TEHAMA – TBC) na Lutengano Haonga (Mwandishi wa Habari Mwandamizi – TBC).

 

Ni mtihani mzito kwa wana familia wenzangu wa TBC. Laleni salama Kaka zangu, kamwambieni Marin Hassan kuwa ARIDHIO inachanja mbuga.”

 

Marehemu Joseph Bernward Kambanga atazikwa leo saa 4 asubuhi, Mloganzila. Ndugu wachache tu wataruhusiwa kuhudhuria mazishi ikiwa ni pamoja na mke wake na watoto wake. Wizara ya Afya itaratibu mazishi yake.

 

Leave A Reply