TARAJI HENSON MIMBA NDII!

Image result for Taraji P. Henson

Taraj P. Henson

NANI alikwambia ukianza kuzeeka ngumu kuzaa? Sikia hii; Staa wa Tamthiliya ya Empire anayetumia jina la Cookie, Taraj P. Henson licha ya kugonga miaka 47, anadaiwa kunasa ujauzito wa mumewe, Kelvin Hayden.  Mtandao wa Media Take Out ‘MTO’ umebumburua ishu hiyo baada ya mchumba wa Taraj kuonekana kuwa naye kwa karibu sana na wakati mwingine kumzuia kutumia kilevi.

Pia, kwa mujibu wa mtu wa ndani wa Taraj akizungumza na mtandao huo alisema, juzikati katika sherehe za US Open alithibitisha kwa vitendo kunasa ujauzito. “Ni kweli Taraj ni mjamzito maana hata pombe hatumii kwa sasa japo kilikuwa ni kilevi chake kikubwa kila mara. Amekuwa akibadilika sura na mwili tofauti na alivyokuwa zamani,” alisema mtu huyo.

 

Loading...

Toa comment