The House of Favourite Newspapers

TARATIBU ZAHERA USIKUBALI KUWA SPIKA YA WENYE CHUKI

KUNA mawazo mabaya sana ambayo wamekuwa nayo wanadamu wengi, kuamini hivi ukiogopwa basi wewe ni mkubwa sana. Hauhi- taji kuogopwa ili kudhihirisha ukubwa wako, badala yake ufanisi wa nafasi unayoitu- mikia ndiyo unaweza kukufanya uujue uku- bwa wako.

 

Lakini hata ukiwa mkubwa, haupaswi kuutumia vibaya ukubwa huo kwa kuwa kama unakwenda nje ya njia sahihi, kuna siku utapotea njia. Nimekuwa kati ya watu ninaofurahishwa na aina ya ufundi wa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera na nimeeleza mara nyingi sana.

 

Huenda ni kati ya waliowahi kuamini hivyo ingawa sasa taratibu ninaanza kutoka huko, nitakueleza kwa nini. Kazi namba moja ya kocha ni kufundisha mpira na kuipa timu yake mafanikio. Kocha zaidi anapaswa kuzungumzia ufundi na mipango ya kikosi na ndiyo asili ya neno kocha lililotoholewa kutoka katika neno la Kingereza ‘coach’ ambayo inajenga coaching ambayo ni ufundishaji.

 

Niliona kivideo kifupi kikisambazwa mitandaoni na mtandao wa Yanga ikawekwa, kwamba Zahera anakanusha kwamba hawajazungumza na Tuyisenge na Gazeti la Championi limeandika uongo kabisa. Hii ni siku chache baada ya Yanga tena kukanusha hawakuwahi kupata fedha kama tulivyoandika.

Wakati huo kuhusiana na fedha, stori ilitoka Yanga na aliyehojiwa alikuwepo na mwisho alikiri ni kosa na kuitoa ile video kwa kuwa kilichoandikwa ni alichosema.

 

Lakini mwisho ikaonekana kusema wana fedha, watu hawatachanga michango, hivyo ikatakiwa kukanusha ili watu waendelee kuchanga. Sasa juzi, Zahera naye amekanusha, akisema Championi limeandika uongo, Yanga hawajamsajili Tuyisenge. Kitu ambacho ni ukosefu wa busara kwa kiwango cha
spika YA WENYE CHUKI juu sana.

Kwanza Championi halikuwa limeandika kuhusiana na Tuyisenge amesajiliwa Yanga. Championi liliandika kuhusiana na wakala wa Tuyisenge ambaye alikuwa akieleza kuzungumza na Yanga na kuwapa masharti, wakitekeleza mshambuliaji huyo nyota wa Gor Mahia atatua Jangwani.

 

Kazungumza wakala wa mchezaji, anakanusha kocha Zahera? Ninaamini Zahera si mtu mwenye nia mbaya, lakini watu wanaomzunguka kwamba wamekuwa wakimjaza maneno wengine kwa maslahi yao binafsi, huenda waliwahi kukosolewa na gazeti hili au tunayajua madudu yao.

Wako walioniambia kwamba mtu anayeitwa Chicharito ndiye amekuwa akimjaza kocha maneno, hafurahishwi anavyoshirikiana na gazeti hili ambalo limekuwa likimpa ushirikiano kuliko chombo chochote cha habari, hivyo hata maneno hayo ya usajili, Zahera hakuwa ameona gazeti na akaelezwa tu naye akajibu.

 

Sitaki kuingia huko, sitaki pia kuamini kama Chicharito ana hizo tabia lakini mara zote uongo au tabia ovu hujitenga na wema, kuna siku itafi kia na mambo yatajidhihirisha na ukweli utakuwa hadharani. Kwa Zahera anapaswa kujua kwamba mara zote amekuwa akipigiwa na kuzungumza mambo kadha wa kadha, vipi ingekuwa kazi kumpata kuhusiana na usajili? Kwa kuwa alikuwa amezungumza wakala wa Tuyisenge, kama haikuwa sawa, yeye ndiye angesema na si Zahera.

 

Na hakuna sehemu iliyosema yeye Zahera amemsajili mchezaji, hivyo kukanusha suala la “kusinya” ilikuwa ni kukanusha ambacho hakikuwepo kwenye gazeti. Huenda wanaomjaza maneno Zahera wa
naamini anahofi wa, huenda kwa kuwa mashabiki wengi wa Yanga wanamuunga mkono.

 

Lakini wanajua kuwa wanachangia kuiporomosha heshima yake kwa kuwa muda mwingi anazungumza mambo yasiyomhusu kwa kuwa yeye si msemaji wa Yanga.

 

Ndiyo maana mwanzo nikaanza na kumshauri, zaidi ajikite na masuala ya timu hasa yake ya ufundi kuhusiana na kikosi chake kinacheza namna gani na nini cha kufanya baada ya kuwa kinapoteza mwelekeo mwishoni mwa ligi kufuatia kufanya vema mwanzoni.

 

Sisi tunajiamini, tunajua wako wanaotuamini na tutaendelea kufanya kazi yetu bila ya woga wa mtu yoyote yule. Anayejaribu kututisha kwa kuionyesha jamii sisi ni wabaya kwa lazima, hatuwezi kukaa kimya. Tutaendelea kuwaheshimu wale wanaotuheshimu. Tunakiri, tunaweza kukosea lakini umakini wetu upo juu na tunajua kila tunachokifanya na stori bomba na za uhakika tutaziandika bila ya woga hata kidogo. Ukisema Yanga, tumeshirikiana nayo kwa zaidi ya miaka 20, kwa zaidi ya makocha 50.

 

Tunajua hata Zahera tunaheshimiana naye lakini anapaswa kutuheshimu pia na kama haitakuwa hivyo, basi hatutamheshimu pia. Mwisho nimshauri Zahera, asikubali kujazwa maneno akageuka kuwa spika. Ndani ya Yanga pia kuna watu wasiopendana ambao wangependa kuona wasiowapenda hawapendwi pia.

 

Kwa kuwa sauti ya Zahera inaweza kusikika vizuri zaidi, basi wanataka kuitumia kufi kisha ujumbe wao wakiwa wamejifi cha. Zahera asikubali kuambiwa kila jambo basi akakubali kuzungumza.

 

Vizuri kuchuja maneno kwanza. Kama unaambiwa Saleh Ally alitusaliti, kabla ya kusema, muite na uzungumze naye ili kujua hali halisi badala ya kutoa maneno ambayo baadaye inakuwa vigumu “kuyameza” tena. Hii ikiendelea itavunja kabisa heshima yako mwishoni.

Makala-Bongo na  SALEH ALLY

Comments are closed.