The House of Favourite Newspapers

TASAC Yang’ara Tuzo Za NBAA Kushika Nafasi Ya Kwanza Kwa Mashirika ya Umma ya Udhibiti Uandaaji Bora wa Hesabu

0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Jamal Kassim Ali akimkabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza katika kipengele cha Taasisi za Udhibiti wa Umma Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Pascal Karomba katika hafla ya utoaji wa Tuzo za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC). Pascal  Karomba akiwa katika picha na wafanyakazi wa TASAC kwenye tuzo za NBAA jijini Dar es Salaam.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) yangara nafasi ya kwanza kwa Mashirika ya Umma ya Udhibiti katika uandaaji bora wa Hesabu mwaka 2022.
Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

TASAC tangu ilipoanzishwa imekuwa ikishikiria nafasi mbalimbali katika Tuzo hizo za NBAA
TASAC imeshika nafasi ya kwanza ya uwasilishwaji bora wa hesabu mwaka 2022 ikishindanishwa na mashirika mengine ya Umma ya Udhibiti wakitumia viwango vya kimataifa vya kutayarisha hesabu

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) , Pascal Karomba amesema ushindi huo umewapa chachu ya kuendelea kuboresha utendaji wake katika maeneo wanayosimamia na utoaji wa huduma bora zinazokidhi viwango wa ndani na nje ya nchi.

“Ushindi huu unatoa ujumbe wananchi kuwa tunanachosimamia kipo salama na fedha zao hakuna zilizopotea na tutaongeza nguvu zaidi kuhakikisha tunakuwa kioo bora kwa wananchi,mtu sasa akiagiza mbolea au mchele kutoka nje kupitia bandari zetu awe na uhakika itafika salama” alisema.

Amesema shindi huu si wa mara ya kwanza kwa Shirika kuibuka kidedea na kufanya kuendelea kujiweka imara zaidi.

Karomba amesema mafanikio hayo yameendelea kuchochea kuimarika kwa utendaji ndani ya taasisi hiyo.

Leave A Reply