The House of Favourite Newspapers

TASWIRA YA MSIBANI NYUMBANI KWA  AGNES MASOGANGE

Msanii za muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja akiwa msibani hapo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni msibani hapo.
Baadhi ya ndugu, jamaaa na marafiki wakiwa katika huzuni msibani hapo.
Taswira mbalimbali za msiba huo.
Nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, Agnes Gerald ‘Masogange’.

 

 

KUELEKEA kifo cha mwanadada aliyekuwa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia jana jioni, baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza nyumbani alipokuwa akiishi msanii huyo Makongo Juu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa wafiwa.

 

Taarifa kutoka kwa dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Flora alisema kuwa taratibu za kutoa heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika kesho Jumapili na mwili wa ndugu yao utasafirishwa siku hiyo kuelekea Mjini Mbeya.

 

Kwa upande wake msanii wa Bongo Fleva, Abdulazizi Chende ‘Dogo janja’ amesema kuwa kifo cha Agnes ni pigo kwa jamii kwani alikuwa bado kijana mdogo na alikuwa akitegemewa na familia hivyo kuondoka kwake kumeacha simanzi nzito kwa wasanii na majirani zake kwa ujumla.

 

Na Denis Mtima/GPL

 

Comments are closed.