Tatizo la Endometriosis (Hitilafu ndani ya kizazi)-2

hemorrhoids-during-pregnancyMpenzi msomaji wa makala haya, leo tunaendelea na mada yetu inayoelezea kuhusu hitilafu ndani ya kizazi ili upate elimu zaidi uweze kujifunza.

Mfumo wa kinga wa mwili

Hitilafu katika mfumo wa kinga ya mwili, unaweza kusababisha kushindwa kwa mfumo huu kuondoa seli na tishu za ukuta wa kizazi zinazojijenga nje ya kizazi. Wanawake wenye udhaifu huu wa kinga ya mwili huwa rahisi kupata ugonjwa, na aina fulani za kansa huwa zinawapata wanawake wengi wenye Endometriosis.

Mfumo wa homoni

Homoni ya Ostrogen ndiyo ambayo huchochea zaidi maradhi haya, na homoni hii hutengenezwa kwa wingi katika umri wa ujana wa mwanamke. Ndiyo maana kwa wale wanawake wa makamo wenye ukomo wa hedhi Menopause, matatizo haya ni nadra au humalizika kabisa. Lakini bado kuna tafiti nyingi zinazoendelea kuchunguza mfumo wa homoni na jinsi unavyosababisha Endometriosis.

Operesheni ya uzazi

Operesheni za sehemu za tumbo, hususan ya tumbo la uzazi wakati wa kujifungua Cesarean Section na operesheni ya kuondoa kizazi Hysterectomy zaweza kusababisha tishu za ukuta wa uzazi Endometrium kupelekwa sehemu nyingine ya mwili kwa bahati mbaya.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

MWISHO.

Toa comment