The House of Favourite Newspapers

Tatizo la Endometriosis (Hitilafu ndani ya kizazi)

0

Karibu msomaji katika ukurasa huu ambao umekuwa ukikupa maarifa muhimu ya afya zetu. Leo tutaangalia tatizo la Endometriosis. Neno hili huenda ni mara ya kwanza kulisikia au umekuwa ukilisikia na huna ufahamu nalo vizuri. Kupitia makala haya utapata maarifa muhimu juu ya tatizo hilo.

Kwanza huu ni ugonjwa unaowapata wanawake ambao unaambatana na magonjwa ya mfumo wa homoni na mfumo wa kinga ya mwili, ambapo seli na tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa uzazi (Endometrium), zinajijenga na kukua nje ya tumbo la uzazi.

Seli na tishu hukua na kujificha katika eneo la nyonga (Pelvis), tumbo la chini (Abnomen) na kwenye ovari na ni mara chache ugonjwa kusambaa kwenye viungo vingine zaidi ya nyonga.

Endometriosis hutokea pale seli na tishu zinapojijenga nje ya tumbo la uzazi na seli hizo na tishu zinakuwa na tabia ya kawaida ya kujijenga na kuongezeka unene, na kubomoka wakati wa mzunguko wa hedhi kama zile zilizojijenga ndani ya mfuko wa uzazi.

Lakini tofauti ni kwamba seli hizi na tishu zilizobomoka na zilizo nje ya tumbo la uzazi, hazitaweza kutoka nje kama damu ya hedhi anayopata mwanamke mwanzo wa mzunguko mpya.

Endapo tatizo hili litaathiri ovari, zaweza kusababisha uvimbe (kwa kitaalam unajulikana kama Endometriomas). Tishu jirani na uvimbe nazo zaweza kuathirika na kupata kovu  au tishu kushikamana isivyo kawaida. Hii huweza kusababisha hata kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai ya uzazi.

Hakuna sababu thabiti kuonesha ni nini hasa kinachosabisha ugonjwa huu, lakini zifuatazo ni sababu zinazoweza kusababisha  ugonjwa huu:-

Sababu za kigenetiki-ugonjwa huu huweza kuwa katika familia fulani, na vinasaba vya ugonjwa vyaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Matatizo katika mtiririko wa hedhi- mtiririko wa kinyumenyume wa hedhi (Retrograde Menstrual Flow) ndiyo sababu kubwa ya mwanamke kupata ugonjwa huu, hii ina maana kwamba mtiririko wa hedhi wa tishu za ukuta wa kizazi uliobomoka hurudi na kuingia katika mirija ya mayai na husababisha tatizo kusambaa katika viungo vingine  kama nyonga.

Leave A Reply