Tatizo la kuharibika kwa ujauzito

recurrent_miscarriageNATUMAINI msomaji wangu utakuwa mzima wa afya, nikukaribishe katika mada ya leo. Leo tunaanza kuangalia tatizo linaloisumbua jamii yetu na dunia kwa jumla.

Kuna tatizo la wanawake wengi wajawazito mimba zao kuharibika na kusababisha wengi kuanza kutafuta mchawi ni nani. Wengi huwa wanaanza kuulizia historia za wenzi wao ili wajue kama kuna mtu amemroga kwa sababu ya wivu wa yeye kuolewa na mambo mengine kama hayo.

Nianze kwa kuliweka wazi hili kwamba, zaidi ya asilimia hamsini ya mimba zote zinazoharibika wanawake wenye mimba hizo hawajui. Hivyo wanaanza kutafuta njia za kubeba ujauzito kumbe ana uwezo wa kubeba ujauzito, lakini kuna matatizo yanayosababisha ujauzito huo kutoka. Hili linapelekea wanawake wengi kujihisi kuwa wao ni wagumba kumbe ukweli haupo hivyo.

Tatizo la kuharibika mimba kitaalamu huitwa ‘Recurrent pregnancy loss’. Mwanamke hujitahidi kubeba ujauzito lakini inakuwa ngumu ujauzito kukua hadi kufikia akafanikiwa kujifungua salama.

Tatizo hili kama nilivyosema linawatesa wanawake wengi sana na kusababisha kukosa raha maishani mwao. Kumbe tatizo hili linatibika na mwanamke husika akarejea katika hali ya kawaida.

Athari za tatizo hili zimekuwa zikiongezeka kila siku kwa kusababisha kuzorota kwa afya ya mama kutokana na mimba kuharibika mara kwa mara lakini pia humwathiri kisaikolojia kwa kutopata watoto.

Na tatizo hili linachangia pia mwanamke kuwa mgumba.

Kipindi cha ujauzito huchukua majuma arobaini kuanzia mimba inapotungwa hadi mama anakuja kujifungua mtoto kamili.  Mtoto kamili na mwenye afya njema huzaliwa katika uzito wa kilo kuanzia mbili na nusu.

Chini ya uzito huu ni watoto wenye matatizo na wanakuwa katika uangalizi maalumu hospitali, chini ya usimamizi wa madaktari wa watoto.

Kipindi cha ujauzito pia hugawanywa katika vipindi vitatu vilivyo sawa miezi mitatu mitatu ambavyo kitaalamu huitwa ‘Trimesters’,  kigezo kinachotumika kugawa vipindi hivi ni matukio yanayofanyika katika muda husika.

Kipindi cha uumbaji

Kipindi hiki huanza tangu mimba kutungwa mpaka miezi mitatu ya awali. Katika kipindi hiki ndipo viungo vya mtoto vinapoumbwa na kukamilika. Mimba inayoumbwa ikiwa na kasoro basi  mwili wa mama unaofanya kazi vizuri huitoa wenyewe hapa tunaona ndiyo mimba inayotoka kabla ya miezi mitatu. Vyanzo vyake huwa ni nadra kutibika.

Vipo vyanzo vingi vinavyosababisha mimba changa ziwe zinatoka, vyanzo hivi ni rahisi kugundulika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na matibabu.

Cha kuzingatia hapa ni kwamba mimba nyingi zinazotoka katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kwanza mara nyingi chanzo huwa ni  mimba yenyewe.

Kuna wanawake wengi wana matatizo haya na hawajui kama tatizo hilo wanalo na wanaweza kutibiwa badala yake wanakazana kutafuta ujauzito badala ya kutafuta njia za kutatua tatizo hili la ujauzito kuharibika.

Kama una tatizo hili la ujauzito kuharibika au umetafuta ujauzito kwa muda mrefu bila kufanikiwa ni vema ukatembelea katika vituo vyetu ili ufanyiwe uchunguzi na kupata matibabu ya tatizo lako.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya, nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.


Loading...

Toa comment